MIRADI YA ZAIDI BIL 2 YATEMBELEWA NA TIMU YA UFUATILIAJI NA TATHIMINI YA MKOA, WILAYANI NACHINGWEA.
Timu ya ufuatiliaji na tathimini ya Mkoa wa Lindi imefanya ufuatiliaji na tathimini ya miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Nachingwea leo Oktoba 10, 2025 ambapo miradi yenye thamani ya zaidi ya Bilioni mbili imetembelewa katika Tarafa ya kilimarondo na Naipanga. Timu hiyo ambayo imeongozwa na katibu Tawala Msaidizi Mkoa seksheni ya Mipango na uratibu Ndugu Juhudi Mgallah akiambatana na wataalamu kutoka mkoani na Halmashauri, wamefanya ufuatiliaji wa pamoja na tathimini katika miradi ifuatayo; ujenzi wa shule Tatu za sekondari ambazo kila moja imegharimu zaidi ya Milioni 560, Shule hizo ni Shule ya Sekondari Mtuanana, Shule ya Sekondari Chiumbati Shuleni na Shule ya Sekondari Amani, umaliziaji wa Nyumba ya Afisa Tarafa ya kilimarondo Milioni 35, ujenzi wa Nyumba ya Mwalimu Shule ya Sekondari kilimarondo Milioni 37, ujenzi wa Mabweni mawili yenye matundu 16 kwa thamani ya Milioni 283 na ujenzi wa mabweni mawili bila choo kwa thamani ya Milinioni 256. Aidha, timu hiyo inatarajia kuendelea na ufuatiliaji siku ya pili Oktoba 11, 2025 katika wilaya hiyo na baadae kutoa mrejesho wa pamoja kwa ajili ya kuongeza ufanisi katika kufanikisha miradi kwa viwango vinavyohitajika.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.