Mkoa wa Lindi umekua mwenyeji wa Kongamano la Wanawake Kanda ya Kusini ulioongozwa chini ya Kauli mbiu isemayo "Ushiriki na Mchango wa Wanawake katika kukuza Maadili, Uzalishaji na Kuongeza Mnyororo wa Thamani ya Mazao"
Akitoa taarifa mbele ya Mgeni rasmi wa Kongamano hilo ambae ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack amesema lengo la kufanya makongamano ni kutathimini utekelezaji wa ajenda ya usawa na kijinsia, haki na uwezeshaji wanawake katika maswala ya maendeleo kijamii, kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni nchini.
Aidha, katika kongamano hilo la maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani Marchi 6,2025 ambapo ngazi ya kanda yamefanyika wilayani Nachingwea Mkoani Lindi limeongozwa na mada ya malezi, uzalishaji na Uongezaji wa mnyororo wa thamani ya mazao yanayozalishwa na wakulima wakiwemo wanawake.
Mada ya uongezaji wa mnyororo wa thamani katika mazao inatokana na sifa ya mikoa ya kusini hususan Lindi kuongoza katika maswala ya kilimo cha mazao ya kimkakati na ya biashara ikiwemo Korosho, Ufuta, Mbaazi na Choroko.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.