Mkuu wa Mkoa wa Mtwara na Mgeni Rasmi katika sherehe za Uzinduzi wa Maonyesho ya Nanenane Kanda ya Kusini Mhe. Kanali Patrick Sawala akitembelea mabanda mbalimbali ya Halmashauri na Taasisi zinazoshiriki katika maonyesho hayo yanayofanyika katika viwanja vya nanenane Ngongo- Halmashauri ya Manispaa ya Lindi.
Kanali Sawala amejionea shughuli mbalimbali zinazofanywa zinazohusisha uzalishaji katika sekta za Kilimo, Ufugaji na Uvuvi pamoja na kazi za ubunifu na uongezaji thamani wa mazao yanayotokana na sekta hizo zinazofanywa na wajasiriamali kutoka katika Halmashauri zinazoshiriki.
Aidha, Kanali Sawala amejionea teknolojia mpya za uzalishaji wa mbegu bora, mbinu za kupambana na magonjwa yanayoshambulia mazao ya biashara hususan korosho, mbinu za uzalishaji wa mazao ya chakula pamoja na teknolojia mpya za kisasa zinazotumika katika shughuli za kilimo zinazosaidia kupatikana kwa mazao mengi, yenye ubora na tija kwa mkulima.
Kauli mbiu ya Maonyesho ya Nanenane 2025 inasema "Chagua viongozi bora kwa maendeleo endelevu ya kilimo, Mifugo na uvuvi 2025"
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.