Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Kanali Patrick Sawala akiongoza kikao cha Nne cha kamati ya maandalizi ya Maonesho ya Nanenane kanda ya kusini leo Julai 24, 2025 amewataka kamati ya maandalizi na taasisi shiriki kuhakikisha maonesho ya mwaka 2025 yanaleta yanakuwa mazuri, yawe na matokeo chanya pamoja na majibu ama suluhu ya changamoto mbalimbali za wananchi.
" Kwa mwaka huu tuwe wa utofauti , wananchi wanataka kuona vitu vipya na kupata majibu ya changamoto zao mbalimbali katika sekta za kilimo, uvuvi ,ufugaji na kujifunza teknolojia mpya za kisasa zitakazo weza kuwasaidia kusonga mbele na kujikwamua kiuchumi "
Akisisitiza hoja hiyo Mhe. Sawala amezitaka taasisi na mashirika yanaendelea kujiandaa vizuri pamoja na kufanya usafi wa mazingira ya maeneo yao kabla ya tarehe 28 Julai 2025 .
Mhe. Sawala amesisitiza wananchi waendelee kuhamasishwa umuhimu wa maonesho hayo kwa kuwashirikisha maafisa Mawasiliano wa Halmashauri na waandishi wa habari ili wananchi ambao ndiyo walengwa wa Nanenane waweze kushiriki kwa wingi.
Awali, Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mhe. Hassan Ngoma kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack ameitaka kamati ya maandalizi kufanyakazi kwa ubunifu mkubwa kuepuka kufanya kazi kwa mazoea ambako hakuvutii ikiwemo aina za burudani ambazo zimekuwa zikitolewa .
Kauli mbiu ya maonesho ya mwaka 2025 inasema " Chagua viongzoi bora kwa Maendeleo ya Kilimo, Uvuvi na Ufugaji 2025 "
Akihitimisha kikao hicho, Mhe. Sawala amewataka wajumbe ambao hawajalipa ada ya ushiriki wa maonesho hayo kulipa ada ya ushiriki kabla ya Julai 28, 2025 .
Kikao cha mwisho kinatarajiwa kufanyika Julai 30, 2025 .
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.