Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Kinga kutoka Wizara ya Afya Dkt.Otilia Gowelle amesema Serikali inatambua mchango mkubwa unaofanywa na Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii, hivyo wanapaswa kuthaminiwa.
Dkt. Gowelle amebainisha hayo leo Septemba 6, 2025 mjini Lindi wakati akizungumza katika Kikao cha Kamati ya Maandalizi kuelekea
hafla ya utoaji wa vyeti na kukabidhi vitendea Kazi kwa wahitimu wa mafunzo kwa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii itakayofanyika tarehe 8, Septemba, 2025.
Aidha, Dkt. Gowelle ameipongeza timu ya Kamati ya Maandalizi mazuri
chini ya Mganga Mkuu Mkoa wa Lindi Dkt. Kheri Kagya .
"Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii wana umuhimu mkubwa, lazima sisi kama Serikali tuendelee kutambua mchango wao kwani wao ndio wanaotusaidia ngazi za chini kabisa kwenye jamii kwenye eneo la afya na kamati inafanya kazi nzuri kuelekea tukio hili muhimu na linapaswa liende kiutendaji zaidi," amesema.
Kwa upande wake Mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt. Ernest Kyungu ameshukuru kwa ushirikiano mkubwa uliofanywa na Kamati ya Maandalizi.
Miongoni mwa watu walioshiriki Kikao hicho ni pamoja na timu kutoka Wizara ya Afya ikiongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Kinga Dkt.Otilia Gowelle, Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma Dkt. Ona Machangu Maafisa kutoka Wizara ya Afya na wawakilishi kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI.
Wengine ni Timu ya Uendeshaji Huduma za Afya Ngazi ya Mkoa (RHMT's), Timu Uendeshaji wa Huduma za Afya Ngazi ya Halmashauri (CHMT's) ,Uwakilishi kutoka Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi, Lindi, Uwakilishi kutoka Shule ya Sekondari Lindi pamoja na Uwakilishi kutoka Mkapa Foundation.
Kikao hicho kimefanyika katika Hospitali ya Sokoine Manispaa ya Lindi.
Wahitimu watatunukiwa vyeti baada ya kufuzu Mafunzo ya Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii waliyosoma katika vyuo vya afya kwa ufadhili wa Serikali kwa kipindi cha miezi sita (6) kupitia Mpango Jumuishi wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii uliozinduliwa na Makamu wa Rais Dkt.Philip Mpango Januari 31, 2024
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.