.
Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametoa zawadi kwa watu wenye mahitaji maalum waishio Rasbura Manispaa ya Lindi ikiwa sehemu ya utaratibu wake na upendo wa kuwakumbuka watu wenye mahitaji maalum .
Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Afya Dkt. Kheri M. Kagya akieleza dhamira ya kuwasilisha zawadi hiyo kwa wenye uhitaji, ameeleza namna ambavyo Serikali inaendelea kuwakumbuka na kuwajali wazee na watu wenye mahitaji maalum. Amesema Serikali ya Dkt. Samia imekuwa ikitoa utaratibu bora wa namna ya kuhudumia makundi hayo hasa katika eneo la afya .
Kwa upande wake Katibu wa itikadi, uwenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Lindi Ndugu Patrick Magarinja, ametoa wito kwa wananchi na wadau mbalimbali kuendelea kutoa msaada na kuwahudumia wenye uhitaji kwani, jukumu la kuhudumia makundi hayo siyo la serikali au taasisi za dini pekee bali la wote.
Akikabidhi mahitaji hayo katika kituo cha Rasbura Manispaa ya Lindi kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Victoria Mwanziva ametumia fursa hiyo kumshukuru Mhe Rais kwa upendo wake kwa wananchi wa Mkoa wa Lindi. Amesema licha ya zawadi hizo, Mhe. Rais amekuwa akitoa fedha nyingi kwa ajili ya shughuli mbalimbali za huduma na maendeleo, katika kipindi cha uongozi wake Mhe. Rais Dkt. Samia ameiletea Manispaa ya Lindi fedha Tsh bil 131.
Wanufaika wa zawadi hizo wametoa shukrani zao kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wanamuombea afya ya kuendelea kuwatumikia wananchi watanzania kwa awamu nyingine .
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.