Wajumbe wa Mkutano mkuu ambao ni watumishi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi wametimiza takwa lao la kikatiba na kidemokrasia la kupiga kura kumchagua Ndug. Ramadhan Hatibu kuwa mwenyekiti wa RAS BOMA SPORTS CLUB kwa awamu nyingine tena .
Ndugu. Ramadhani Hatibu amethibitishwa kuwa mwenyekiti kwa awamu nyingine kwasababu ni mgombea pekee kwa nafasi hiyo .
Mara baada ya kuchaguliwa ndugu Hatibu amewashukuru wajumbe kwa kuendelea kumuamini kwa kipindi kingine cha miaka minne kuongoza klabu hiyo .
Aidha, amewasihii viongozi wote waliochaguliwa kushika nafasi hizo kushirikiana vizuri kuhakikisha dhamira ya uwepo wa klabu hiyo unatimia hasa wa kuhamasisha kila mmoja kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi kwa afya.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.