Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi wamefanya uchaguzi wa uongozi mpya wa timu ya RAS BOMA SPORTS CLUB ikiwa ni takwa la katiba yao inayotaka uchaguzi Mkuu wa uongozi unapaswa kufanyika kila baada ya miaka minne .
Katika uchaguzi huo nafasi ambazo zimegombewa ni nafasi ya Mwenyekiti na Msaidizi wake, Katibu na Msaidizi wake , Mweka hazina , Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa SHIMIWI na Wajumbe Kamati Kuu Tendaji nafasi Tano.
Akitangaza matokeo hayo msimamizi wa uchaguzi huu,Afisa Utamaduni Mkoa Bi. Makalaghe Nkinda kwaniaba ya Afisa Michezo Mkoa wa Lindi,alisema kuwa
nafasi ya mwenyekiti Mshindi ni Ramadhani Hatibu,nafasi ya Mwenyekiti Msaidizi Patrick Maniula,
Bi Makalaghe alisema nafasi ya katibu Mkuu mshindi ni Bi. Zaituni Makate, nafasi ya Katibu Msaidizi mshindi ni Betrice Mwiru,mweka Hazina Ndugu Frank Mtachuba ameibuka mshindi wa nafasi hiyo.
Aidha nafasi ya mjumbe Mkutano Mkuu Taifa SHIMIWI Bi. Neema Mrisho Konzo kuwa mjumbe wa nafasi hiyo na nafasi ya mwisho ni wajumbe tano wa kamati tendaji ambao wamechaguliwa na wajumbe ni Kassim Abeid Nyanga, May Nahumbwa, Josephy Alfred Mwenyo, Theresia Paul Mapunda na Christopher Sebastian Namihambi.
Mara baada ya kutangazwa matakeo hayo , Mwenyekiti amewashukuru wajumbe wa mkutano huo na kuwataka viongozi waliochaguliwa kushirikiana kuhakikisha michezo inafanyika kwa mafanikio makubwa ofisini hapo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.