Katibu Tawala Mkoa wa Lindi Bi. Zuwena omary amekagua ujenzi na ukarabati wa miundombinu mbalimbali inayoendelea kujengwa na kukarabatiwa ikiwemo ukarabati wa jengo la utawala namba Moja na ujenzi wa uzio wa Nyumba ya Mkuu wa Mkoa .
Ukaguzi wa miradi hiyo ameufanya leo Novemba 12, 2025 akiambatana na timu ya wahandisi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wakiongozwa na Mhandisi Godfrey Mlowe. Kwa mujibu wa Mhandisi Godfrey Mlowe ameeleza kuwa hadi sasa ukarabati wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa umefikia 56% huku ujenzi wa uzio wa nyumba ya Mkuu wa Mkoa ukifikia 35% .
Katibu Tawala Bi. Zuwena Omary, mara baada ya kukagua, amesisitiza ukamilishaji wa miradi hiyo kwa wakati huku ikizingatia viwango na ubora . “Hakuna sababu ya kuchukua muda mrefu kukamilisha miradi hiyo, jambo la msingi kuzingatia viwango, vigezo na masharti “ katibu Tawala .
Miradi mingine ambayo inaendelea kutekelezwa pamoja na ujenzi wa uzio wa nyumba za wakuu wa seksheni zilizopo Mitwero ambao unagharimu zaidi ya Milioni 758, uwekaji wa viyoyozi ukumbi Mkubwa kwa thamani ya Mil 118 ambapo zoezi hilo limekamilika 100% na ukarabati wa Nyumba ya kupumzika viongozi kwa thamani ya Milioni 565 ukarabati wake umekamilika kwa 100% . Fedha hizo zote zaidi ya Bilioni 2.3 zimetoka serikali kuu kwa lengo la kuhakikisha wananchi na watumishi wa umma wanaendelea kupata huduma bora katika mazingira rafiki.








Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.