Katibu Tawala Mkoa wa Lindi Bi. Zuwena Omary ambaye ni mwenyekiti wa Baraza la wafanyakazi sekretarieti Mkoa ameongoza kikao cha Baraza hilo leo Januari 21, 2025 kilichofanyika katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa Lindi .
Kikao hicho cha kawaida kinapaswa kufanyika mara mbili kwa mwaka chenye lengo la kuwakutanisha wafanyakazi na mwajiri kujadili masuala mbalimbali yanayohusu kazi, kwa kutumia vyama vya wafanyakazi na vyombo vya ushauri ikiwemo Baraza la wafanyakazi katika kutatua changamoto mbalimbali sehemu za kazi .
Akifungua baraza hilo, katibu Tawala Bi. Zuwena Omary amewashukuru na kuwapongeza watumishi wa umma wa Mkoa wa Lindi kwa kuendelea kutimiza majukumu yao hasa mwaka 2024 , amewasihii kuendelea kufanya hivyo na zaidi mwaka 2025 .
Amesema kuwa kupitia vyama vya wafanyakazi na sheria zilizopo zilrnge kuhakikisha utulivu sehemu za kazi badala ya migogoro.
"Waajiri na wafanyakazi ni lazima sote tutambue kwamba sheria za kazi zimetungwa kwa lengo la kuleta utulivu sehemu za kazi badala ya migogoro isiyo na tija " Bi. Zuwena Omary RAS Lindj.
Kikao hicho kimejumuisha wajumbe kutoka ofisi za wakuu wa wilaya na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.