Kamati ya uratibu Maandalizi ya Maonesho ya Madini na fursa za Uwekezaji Mkoa wa Lindi 2025, imetoa tuzo ya pongezi kwa katibu Tawala Mkoa wa Lindi Bi. Zuwena Omary @jirized kwa kutambua Mchango wake Mkubwa katika kufanikisha maandalizi ya maonesho ya Madini Mkoa wa Lindi mwaka 2025.
Tuzo hiyo imekabidhiwa rasmi leo Agosti 26,2025 na Mwenyekiti wa kamati ya uratibu wa Maonesho hayo Ndugu Mwinjuma Mkungu akiambatana na baadhi ya wajumbe wa kamati. Tuzo hiyo ilitajwa Juni 2025 siku ya killele cha Maonesho ya Madini yaliyofanyika wilayani Ruangwa.
Ndugu Mkungu, amesema kuwa, kamati imetoa tuzo kwa wadau, Mashirika, Taasisi na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack ambaye ndiye mwasisi wa Maonesho hayo ya Mkoa.
“Tunakukabidhi tuzo hii ishara ya kutambua mchango wako na maelekezo yako katika kufanikisha Maonesho ya Madini Mkoa wa Lindi 2025 kufanyika kwa kiwango na ubora mkubwa “ Mkungu .
Kwa upande wake Katibu Tawala Bi. Zuwena Omary amewashukuru wajumbe wa kamati hiyo, kwa kutambua mchango wake katika kufanikisha Maonesho hayo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.