Kwa kuzingatia mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia na mbinu za Kisasa za utendaji kazi, Katibu Tawala Mkoa wa Lindi Bi. Zuwena Omary ametoa rai kwa watumishi wa umma Mkoa wa Lindi kujiendeleza kupata mafunzo mbalinbali iwe ya muda mfupi au muda mrefu .
"Napenda kutoa rai kwenu vyote kuwa kila mmoja wenu anapaswa iwe kwa kujigharamia au kugharamiwa na Serikali ahakikishe anapata mafunzo ya muda mfupi au muda mrefu kwa madhumuni ya kwenda na wakati " Bi. Zuwena Omary Katibu Tawala Mkoa Lindi.
Rai hiyo ameitoa leo Januari 21, 2025 akifungua kikao cha baraza la wafanyakazi Sekretarieti ya Mkoa wa Lindi .
Akisisitiza hoja hiyo ameeleza kuwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa imeweza kugharamia mafunzo ya watumishi 10 wa muda mfupi na watumishi 8 wa muda mrefu.
Ameeleza kuwa kupitia elimu au mafunzo mbalimbali yanaongeza kuwa na ubunifu katika kazi .
"Ubunifu unaweza kupatikana kwa njia mbalimbali pamoja na kujisomea na kujifunza " RAS Zuwena Omary.
Aidha, ameiiagiza idara ya utawala kujipanga na kuandaa mpango endelevu wa kutoa mafunzo kwa watumishi kutegemea na uwezo wa kifedha.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.