Katibu Tawala Mkoa wa Lindi . Bi. Zuwena Omary awataka maafisa wanaosimamia mpango wa TASAF mkoani Lindi kuendelea kuwasimamia wanufaika wa TASAF ili waendelee kujikwamua kiuchumi huku wakiendelea kuifadhi taarifa muhimu za mpango huo ambao umefika tamati.
Wito huo ameutoa Septemba 11, 2025 alipokuwa anafungua kikao cha tathimini cha mpango wa TASAF II, kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi.
Moja ya eneo ambalo amewasisitiza , eneo la mikopo 10% inayotolewa na Halmashauri iweze kusaidia walengwa wa TASAF .
"Rai, yangu tukavitumie vizuri vikundi vya TASAF vilivyoanzishwa, tukavilee, tukavitunze, tukaviimarishe, tuviendeleze na tuviwezeshe viweze kukopa mikopo hii ambayo ipo na vyenyewe viweze kufanya shughuli za ujasirimali " katibu Tawala Bi. Zuwrna Omary.
Ameongeza kuwa kwakuwa fedha za 10% zinaweza kuwa nyingi zaidi ya zile za TASAF ametoa wito kwa maafisa hao kuwaunganisha na mifumo ya elimu ya fedha ili waweze kuwa na uwezo wakusonga mbele .
" vikundi hivi tumejua vimetokea wapi , bado tunahitaji kuviimarisha zaidi kwenye elimu ya fedha kwasababu fedha walizokuwa wanapokea kwenye TASAF ni ndogo na hata miradi ambayo walikuwa wanafanya inawezekana ni midogo sasa wanakwenda, kuna fedha za 10% lakini kuna fedha hizo za mikopo lazima tuhakikishe vikundi hivi tunaviendeleza na kuvipa elimu na usimamaizi wa karibu" Bi. Zuwena Omary .
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.