Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack Leo jumanne Novemba 12, 2024 amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Kampuni ya Jinyimeng Group kutoka nchini China.
Mhe. Telack akizungumza na uongozi wa Kampuni hiyo, amewaeleza fursa zilizopo Mkoa wa Lindi ikiwemo upatikanaji wa madini, bidhaa za kilimo kama vile ufuta, korosho, muhogo, mbaazi na mazao mengine.
Pamoja na uwepo wa fursa hizo, Mhe. Telack ameihakikishia Kampuni hiyo ubora na usalama wa malighafi zinazopatikana Mkoani Lindi.
Aidha, Kampuni hiyo ya kichina imevutiwa na kuonesha nia ya kuwekeza kwenye uzalishaji wa bidhaa za kikemikali ikiwemo mbolea na bidhaa zingine.
Kupitia uwekezaji huo, kampuni imeahidi kutumia malighafi ya zao la muhogo ambalo linalimwa Kwa kiasi kikubwa Mkoani hapa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.