Serikali ya Mkoa wa Lindi imewapokea rasmi madaktari bingwa 47 chini ya mpango wa Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, awamu ya tatu, kwa ajili ya kutoa huduma za kibingwa katika hospitali zote za wilaya ndani ya mkoa huo ambazo zinatolewa kuanzia tarehe 19 hadi 24, 2025 .
Akizungumza wakati wa mapokezi ya madaktari hao, Katibu Tawala Mkoa wa Lindi, Bi. Zuwena Omary, alisema kuwa ujio wa madaktari hao ni sehemu ya jitihada za serikali kusogeza huduma za afya karibu na wananchi, hasa wale walioko maeneo ya vijijini ambako awali walilazimika kusafiri umbali kuoata huduma hizo za kibingwa.
“Huduma hizi zitapatikana katika maeneo saba ndani ya mkoa kwa siku sita mfululizo kuanzia leo. Lengo ni kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma bora na kwa wakati,” alisema Bi. Omary.
Aliongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imekuwa mstari wa mbele kuboresha sekta ya afya kwa kujenga miundombinu ya kisasa, kununua vifaa tiba vya kisasa, pamoja na kuongeza wataalamu mbalimbali wa afya nchini.
Akisisitiza hoja hiyo amewasihii wananchi wa Mkoa wa Lindj kujitokeza kwa wingi kuoata huduma hizo za kibingwa .
Mratibu wa timu hiyo ya madaktari, Dkt. Michael Mbele, alieleza kuwa madaktari hao wamejipanga kikamilifu kutoa huduma zote muhimu za afya kwa wananchi wote, bila ubaguzi, katika hospitali za wilaya walizopangiwa.
“Tumewakilishwa na wataalamu wa kada zote za afya, kuanzia magonjwa ya ndani, watoto, wanawake, upasuaji na hata huduma za kisaikolojia. Huduma zote hizi sasa zitapatikana katika hospitali za wilaya,” alisema Mbele.
Kwa upande wake, Kaimu Katibu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Lindi Dkt. Charles Mtabho amesema kuwa madkatari wa hoa watatoa huduma za kibingwa kwa katika halmashauri zote , huduma hizo pamoja na mifumo ya uzazi, kooa na masikio, magonjwa ya watoto
Wananchi wa Mkoa wa Lindi waliopata fursa ya kuhudumiwa walieleza furaha shukrani kwa serikali, hususani kwa Mheshimiwa Rais, kwa kuendelea kuboresha huduma za afya nchini, hatua ambayo wameitaja kama ya kipekee na ya kupongezwa.
@wizara_afyatz
@ortamisemi
@jirized
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.