Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mh. Zainab Telack amewataka Halmashauri ya Mtama kuhakikisha wanawasimamaia fedha za miradi ya ujenzi wa shule na miundombinu ya elimu.
Mhe. Telack ametoa wito huo mapema alipotembelea kukagua ujenzi wa shule na miundombinu hiyo ya elimu yenye thamani ya Bilioni 7.8
Kati ya fedha hizo, shilingi Bilioni 4.1 zinatoka serikali kuu, bilioni 3 kutoka kwenye Mradi wa Kuboresha Elimu ya Sekondari (SEQUIP), na milioni 719 kutoka kwenye Mradi wa Kuimarisha Ufundishaji na Ujifunzaji kwa Shule za Awali na Msingi Tanzania Bara (BOOST).
Miradi inayotarajiwa kutekelezwa ni pamoja na ujenzi wa shule ya wavulana kanda ya Kiwalala, ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na matundu sita ya choo katika Shule ya Msingi Mahumbika, ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa na matundu sita ya choo katika Shule ya Msingi Chiuta, na ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na matundu sita ya choo katika Shule ya Msingi Mandwanga.
Pia kutakuwa na ujenzi wa Shule mpya ya Msingi Mtakuja, ukarabati wa madarasa matano katika Shule ya Msingi Simana, ujenzi wa Shule ya Sekondari Navanga, na ujenzi wa Shule ya Amali Mpenda.
Miradi mingine ni ujenzi wa madarasa matano katika Shule ya Msingi Simana, ujenzi wa Shule ya Sekondari Mtakuja katika Kata ya Nyangao, ujenzi wa shule mpya ya amali mkoa, na ujenzi wa Shule ya Sekondari katika Kata ya Pangani.
Akizungumza mara baada ya kutembelea na kukagua uendelevu wa miradi hiyo, awali, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Zainab Telack , ametoa wito kwa menejimenti ya halmashauri na mafundi waliopata kazi ya kujenga miundombinu hiyo kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati na ubora .
Mohamed Ismail Mpakatika ambaye ni fundi wa moja kati ya shule zinazojengwa amesema amepokea maagizo ya Mhe. Mkuu wa Mkoa atahakikisha na wenzake wanakamilishe mradi kwa wakati.
Naye Salma B. Ng’ombo amesema fedha ambazo Mhe. Rais amezilete mkoa wa lindi husuani Halmashauri ya Mtama katika Afya na elimunni nyingi sana hawana budi kumshukuru kwa fedha hizo.
@ortamisemi
@ikulu_mawasiliano
@zainabutelacky
@wizara_elimutanzania
@mohamed_mchengerwa
@jirized
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.