Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack amewataka Maafisa Lishe wa Mkoa wa Lindi kutoa elimu ya lishe bora kwa kina mama wajawazito na wanaojifungua.
Mhe.Telack Akizungumza na wadau wa lishe Jana alhamisi kwenye kikao cha mkoa cha tathmini ya lishe amesema wataalam hao wasaidie kutoa elimu hiyo ili watoto wanaozaliwa wapate aina ya chakula kwa kuzingatia umri. Ameongeza kuwa elimu ya msingi kwenye ukuaji wa mtoto inaanzia kwenye unyonyeshaji pindi tu mtoto anapozaliwa.
Mhe. Telack amesisitiza kuwa elimu hiyo itolewe Mkoa mzima ili wazazi waelewe vyakula bora vinavyosaidia ukuaji bora kwa mtoto. Ameongeza kuwa elimu hii itasaidia pia kupunguza tatizo la udumavu na utapiamlo kwa watoto.
Mhe. Telack ametoa wito kwa kina mama wajawazito na waliojifungua kuzingatia elimu ya lishe itakayosaidia uboreshaji wa afya ya mtoto, kujenga ubongo na mwisho kuwa na kizazi Chenye maamuzi sahihi.
Awali Akizungumza mbele ya wajumbe, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Lindi Dkt. Khery Kagya amesema kuwa kwa sasa Mkoa wa Lindi unaendelea kusimamia na kuratibu programu za lishe kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali.
Dkt. Kagya ameongeza kuwa hali ya lishe kwa ujumla sio mbaya ambapo Kwa mujibu wa tafiti iliyofanyika 2018/19 kiwango cha udumavu kilikuwa 23.8 na kiwango Kwa mwaka 2020-22 kiwango cha udumavu ni asilimia 21.3. Takwimu hizi zinaufanya Mkoa wa Lindi kushika namba 4 kwa mikoa inayofanya vizuri katika kupambana na udumavu nchi nzima. Ameongeza kuwa lengo la Mkoa ni kumaliza kabisa tatizo la udumavu kwa watoto.
Akiwasilisha matokea ya hali ya lishe kwa tafiti zilizofanyika, Afisa lishe wa Mkoa Bi. Juliana Benjamin Chikoti amesema tatizo la udumavu na ukondefu linachangiwa kwa kiasi kikubwa unyonyesha mbovu wa watoto, Jambo ambapo linadumaza ukuaji wa ubongo wa mtoto na mwili kwa ujumla.
Kikao cha tathmini ya lishe Kimkoa hufanyika kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali wa lishe ili kufanya tathmini ya hali ya lishe kwa Mkoa mzima na kuweka mikakati ya kukabiliana na changamoto zinazobainishwa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.