Mkuu wa mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack amewataka wakulima mkoani Lindi kutouza mazao yao kwa njia ya ulanguzi na badala yake wanapaswa kuuza mazao yao kwa mfumo rasmi uliowekwa na serikali kwa kuwa upo utaratibu mzuri wa uuzaji wa mazao kupitia soko la ushirika litakalomsaidia mkulima kupata masoko ya uhakika ya kuuzia mazao
Mhe. Telack ametoa Wito huo katika mkutano wa Jukwaa la Ushirika la Mkoa wa Lindi, akisisitiza hoja hiyo amesema seriikali kupitia sera ya mifumo kusomana imeendelea kuboresha mifumo ya upimaji wa mazao ambapo mazao ya wakulima yatapimwa kwa mizani ya kidigitali itakayomwezesha kupokea taarifa za kiwango cha mazao yake kupitia simu ya mkononi na fedha anayopaswa kulipwa hatua itakayoepusha Mkulima kuibiwa mazao yake.
Kwa upande wa Benki ya ushirika, Mhe. Telack ,ameitaka Benki ya hiyo kuingia kwenye Ushindani kwa kuwatembelea wakulima katika vyama vyao ili kujiongezea idadi ya wateja.
Katika hatua nyingine, ameviagiza vyama Vikuu na AMCOS Mkoani humo kufanya maandalizi mapema ya msimu mpya wa zao la ufuta ikiwemo kuandaa vifungashio ili msimu utakapoanza uanze pasipo na changamoto wakati huo wakiendelea kuwahimiza wakulima kuepuka kuuza ufuta wao kwa walanguzi huku akiwaondoa hofu kuhusu bei za ufuta kwani kutokana na mifumo inayotumika sasa inaleta ushindani wa soko.
Aidha amewataka viongozi wa Amcos kuhakikisha mazao wanayoyapokelewa kutoka kwa wakulima yanazingatia ubora ili kulinda soko hasa la ufuta ambao siku chache zijazo minada inakwenda kuanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.