RC TELACK AONGOZA KIKAO CHA WADAU WAKOROSHO LINDI, AWAPONGEZA MAAFISA KILIMO KWA USIMAMIZI.
Mkuu wa mkoa Lindi Mhe. Zainab Telack amewapongeza maafisa kilimo pamoja na maafisa Ushirika kwa kusimamia kilimo mkoani humo.
Pongezi hizo amezitoa leo Julai 2,2025 kwenye kikao Cha wadau wa korosho kikiwa na lengo la kujadili zao hilo Kwa Mkoa wa Lindi kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi.
Aidha amewaomba maafisa kilimo Kwa kuendelea kutoa Elimu na kushawishi Vijana kuweza kujiajiri kwenye sekta ya kilimo Kwani Mkoa wa Lindi una maeneo mengi mazuri kwa ajili ya shughuli za kilimo.
Sambamba na hilo Rc Telack ametoa rai Kwa wakulima kuwatumia maafisa kilimo ili kuepukana na magonjwa ya mikorosho ambayo yanaweza kusababisha kupata mazao yasiyo Bora.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya korosho Tanzania Bw, Francis Alfred amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Kwa kuwapatia wakulima pembejeo za Bure ambazo kwa kiasi kikubwa zimepelekea kuongeza Uzalishaji wa zao la korosho na kusaidia kuboresha maisha ya wakulima wengi Kwa Mkoa wa Lindi na Mtwara.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.