Kamati ya ushauri ya Mkoa wa Lindi (RCC) ikiongozwa na mwenyekiti wake Mhe. Zainab Telack ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi imeona changamoto kubwa ya watumishi wa umma katika sekta ya elimu na afya inayotokana na sababu ya kuhama na kubadilisha kada ya utumishi inavyoathiri utendaji na upatikanaji wa huduma .
Katika eneo la watumishi, kamati ya mkoa imeona kuna umuhimu wa kuandaa utaratibu wa kupata watumishi wakujitolea ili kutatua changamoto hiyo.
"Tunafikiria pia utaratibu ule wa kuwa na watumishi wale waliomaliza ambao wanaweza kujitolea wakapata malipo kidogo kupitia kwenye halmashauri zetu, tunaendelea na mjadala nalo mwisho, tutatoka na wakurugenzi namna gani tunaweza kufanya ili wananchi waweze kupata huduma " Mhe. Zainab Telack.
Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za serikali kwa kipindi cha 2023/2024 na Julai 2024 hadi 2025 katibu Tawala Msaidizi Mipango na uratibu Ndugu Juhudi Mgala ameeleza kuwa pamoja na jitihada kubwa za serikali kuajiri walimu 952 katika kipindi cha miaka 3 , Mkoa umeendelea kuathirika na changamoto ya walimu kuhamia mikoa mingine na kubadilisha kada za kiutumishi .
Ndugu Mgala ametoa mfano kwa kipindi cha mwezi march hadi Desemba 2024 walimu 422 wamepata uhamisho kwenda nje ya mkoa na wengine kubadilisha kada ya utumishi.
Katika hatua nyingine kamati imeshauri TAMESA kuongeza muda wa usafirishaji wa kivuko cha kitunda , badala ya kuishia saa 12 jioni iongezeke muda angalau hadi saa 2 usiku .
"Meneja wa TEMESA angalia uwezekanao wa kuongeza muda wa usafirishaji katika kivuko cha kitunda " Mhe. Telack
Aidha, Mwenyekiti amewasisitiza wajumbe kuendelea kuweka nguvu katika uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara kwani Mkoa unafanya vizuri katika mazao ya mbazi, ufuta na korosho . Akitoa wito huo amewasisitiza kuendelea kutoa elimu ya matumizi sahihi ya fedha wanazozipata wananchi baada ya kuuza mazao yao ili ,ziweze kuleta tija katika maisha yao.
@ortamisemi
@maendeleoyajamii
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.