Mganga Mkuu wa Mkoa wa Lindi Dkt.Herry Kagya amewataka waajiriwa wapya wa kada ya Afya Katika Hospitali ya Sokoine Manispaa ya Mkoa wa Lindi kuzingatia miiko na maadili ya kazi ili kwenda kutoa huduma iliyo bora kwa wananchi.
Ameyasema hayo wakati akitoa mafunzo maalumu kwa waajiriwa wapya wa kada hiyo yalioandaliwa na chuo Cha Afya Cha Lichas yaliyofanyika 15 januari 2025 Katika ukumbi maalumu uliopo Katika hospitali ya Sokoine Mkoani Lindi .
“Tunapotekeleza majukumu yetu, tunayo miiko, nimeambiwa hapa na nimefurahi kwamba siku ya mwisho mtaapa hapa kiapo cha utumishi cha jumla, lakini kwa kada zenu pia mnavyo viapo vyenu, madaktari wataapa, si ndiyo nawauguzi wataapa, twendeni tukaviheshimu, tukaviishi viapo hivi “Dkt Kagya.
Aidha Dkt Herry amesema mafunzo hayo yamejumuisha waajriiwa wapya 150, kati ya hao 132 watatumika kutoa huduma hospitali ya Mkoa Sokoine na 18 wameajiri kwa ajili ya chuo Cha Afya Lichas kilichopo jirani na hospitali hiyo.
Amewasistiza juu ya kuwasilisha changamoto zao watakazokumbana nazo wakati wa kutekeleza majukumu yao kwa viongozi ambao wanahusika Katika vitengo vyao endapo kutakuwa na ulazima wa kufika kwao.
Ametumia fursa hiyo kumshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa ajira hizo hususani kada ya afya .
Kwa upande wake afisa muuguzi wa ajira mpya hospitali ya sokoine ,Asteria David ,ameshukuru serikali ya awamu ya 6 kwa kuwapatia ajira kwa wingi Katika fani ya Afya ambao watakwenda kuwatumikia wananchi .
‘’Naishukuru sana serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya awamu ya sita kwa kutupatia nafasi nyingi sana za ajira kwa sekta ya afya ambazo haijawahi kutokea, tunamshukuru sana na kumpongeza mama samia silihu Hassan kupitia katibu mkuu wizara ya afya na utumishi wa umma’’amesema asteria
Kadhalika Asteria ameshukuru uongozi wa hospitali ya sokoine kwa mapokezi mazuri kwani imewaongezea ufanisi wa kwenda kutumikia fani Yao ili kuwa watumishi bora watakao jali na kutimiza majukumu Yao
Kupitia mafunzo hayo Asteria amesema yamewaongezea uwezo wa kutambua haki na wajibu kama mtumishi wa umma na kuahidi kutoa huduma bora kwa kuwatumikia wananchi wa mkoa wa lindi Katika hospitali ya sokoine
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.