Shule ya Sekondari Nachingwea imeibuka kidedea katika Mashindano ya 15 ya Young Scientist Tanzania (YST) yaliyofanyika tarehe 18 Septemba 2025 katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ukumbi wa New Library.
Katika mashindano hayo, kulikuwa na jumla ya miradi 45 kutoka shule mbalimbali nchini. Nachingwea Sekondari iliuwakilisha vyema Wilaya ya Nachingwea pamoja na Mkoa wa Lindi kwa ubunifu wao wa kipekee.
Mradi wao ulihusu namna ya kudhibiti uvamizi wa tembo katika mashamba kwa kutumia njia za asili. Mradi huu uliwasilishwa chini ya kundi la Climatic Change and Environmental Science na uliibua mvuto mkubwa
kutokana na suluhisho lake la moja kwa moja kwa changamoto ya wanyama pori kuvamia maeneo ya wakulima.
Wanafunzi waliobuni na kuwasilisha mradi huu ni Igalu Haji Mussa na Hiyari Hamisi Namkuva, wote wakiwa ni wanafunzi wa Kidato cha Sita. Waliandaliwa na kuongozwa na mwalimu wao, Nehemia Philibert Mayala.
Kutokana na ubunifu wao wenye manufaa kwa jamii, walipewa Tuzo Maalumu iitwayo Special Silver Award.
Tuzo hiyo imetolewa na wadhamini wa mashindano hayo kama ishara ya kutambua kazi yao bora na mchango wao katika sayansi na mazingira.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.