Lindi, 2 Agosti 2025 – Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Mhe. Mwanziva, ametembelea mabanda mbalimbali ya washiriki wa Maonesho ya Nanenane Kanda ya Kusini yanayoendelea katika viwanja vya Ngongo, Manispaa ya Lindi.
Akiwa ni mgeni rasmi katika siku ya pili ya maonesho hayo, DC Mwanziva alipata nafasi ya kujionea ubunifu na teknolojia mbalimbali zinazotumika katika sekta za kilimo, mifugo na uvuvi kutoka kwa taasisi, mashirika na vikundi vya wakulima wanaoshiriki.
Katika hotuba yake fupi, Mhe. Mwanziva aliwapongeza washiriki wote kwa maandalizi mazuri na alieleza kuwa maonesho hayo ni jukwaa muhimu kwa wakulima kujifunza mbinu bora za kisasa zitakazochochea uzalishaji na kuongeza tija.
“Mwendelee kutumia fursa hii kujifunza na kubadilishana uzoefu, kwani serikali ina dhamira ya dhati ya kukuza kilimo chenye tija kwa vijana na wanawake,” alisema Mwanziva.
Maonesho ya Nanenane kwa Kanda ya Kusini yanatarajiwa kuhitimishwa tarehe 8 Agosti 2025, yakihusisha washiriki kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.