SERIKALI INATAMBUA UMUHIMU WA KUKUZA USAWA WA KIJINSIA NA UWEZESHAJI WANAWAKE-MAJALIWA
Kuelekea Siku ya Wanawake Duniani, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) leo Machi 6, 2025 amezungumza na wanawake katika Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Kanda ya Kusini, yanayofanyika katika viwanja vya Maegesho, Nachingwea mkoani Lindi.
Akifungua kongamano hilo, Mhe. Majaliwa amesema kuwa Serikali inatambua umuhimu wa kukuza usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake kama njia mojawapo ya kuimarisha ustawi na kufikia maendeleo jumuishi na endelevu.
Aidha, Waziri Mkuu amewataka wanawake kuendelea kuhamasishana na kutumia fursa zilizopo katika maeneo yao ikiwemo mikopo inayotokana na halmashauri (10%) na taasisi za kibenki kwa kuzingatia mikopo yenye masharti nafuu ili kutoathiri maendeleo na mienendo ya maendeleo ya mwanamke na mjasiriamali.
Kupitia kongamano hilo lililowakutanisha wanawake kutoka Mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma, wanawake wametakiwa kuanzisha viwanda vidogovidogo vya uchakataji ili kuongeza mnyororo wa thamani wa mazao ya kilimo wanayoyazalisha ili kujiongezea kipato kupitia kuuza bidhaa badala ya malighafi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.