Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania Bw. Francis Alfred, akiwasilisha taarifa ya mpango wa ugawaji wa Pikipiki na vishikwambi kwa maafisa ugani 152 Mkoa wa Lindi, ameeleza kuwa lengo la serikali kugawa Pikipiki hizo kwa maafisa ugani kuwarahisishia namna ya kuwafikia wakulima kwa wakati ili kuweza kuleta tija na ongezeko la uzalishaji wa zao la korosho nchini kupitia programu ya Jenga Kesho iliyo Bora (BBT)
Bw. Francis Alfred ameeleza kuwa mpango huo unalengo la kuongeza uzalishaji kufikia Tani Laki 7 katika msimu wa 2026 na Tani Mil 1 ifikapo mwaka 2030. Katika kufanikisha hilo serikali imetenga kiasi cha Bil. 8 ili kutekeleza mpango huo na kuajiri maafisa ugani 500 nchi mzima na kuwawezesha vitendea kazi ili kurahisisha mazingira ya utendaji wa kazi na kufikia lengo la mpango wa BBT.
Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Lindi Bw. Francis amewataka Maafisa Ugani wa BBT kushirikiana kwa ukaribu na Maafisa Ugani wa Halmshauri, Vyama vya Ushirika na Wataalam wengine wa Kilimo kusimamia uzalishaji wa zao la korosho na kutoa ushauri wa kitaalamu kwenye mazao mengine ili kumnufaisha mkulima.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.