Katika kutekeleza kwa vitendo sera ya uboreshaji na uongezaji fursa ya kupata elimu katika ngazi mbalimbali nchini , serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt . Samia Sulubu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imejidhirisha kwa vitendo kwa kujenga miundombinu mbalinbali ya shule za msingi na sekondari yenye lengo la kuhkiisha idadi ya watoto wenye umri wa kenda shuke wanapata elimu bila kikwazo .
Moja ya jitihada na nia hiyo thabiti ni ujenzi wa shule mpya ya sekondari ya wavulana inayojengwa katika kijiji cha Kiwalala , kata ya kiwalala halmashauri ya Mtama Lindi.
Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameleta fedha kiasi cha Tsh Bili 4.1 (Bilioni Nne na Milioni Mia Moja bila senti ) .
Fedha hizi zinatoka serikali kuu kupitia mradi wa SEQUIP (Secondary Education Quality Improvement Programme ) ili kuboresha mazingira ya ujifunzaji na ufundishaji na kuwawezesha watoto kupata elimu katika mazingira bora na wezeshi .
@lindi_rs_
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.