Katika kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan , Benki ya CRDB imekabidhi mifuko 100 ya saruji shule ya Sekondari Lindi Wasichana iliyopo kata ya Kilangala Jimbo la Mchinga Halmashauri ya Manispaa ya Lindi, kwaajili ya Ujenzi wa uzio shule hiyo.
Akiongea na wanafunzi wa shule hiyo mara baada ya kukabidhi mifuko hiyo meneja wa CRDB kanda ya Kusini Bwana Denis Mwoleka amesema, saruji hiyo ni muendelezo wa mambo mbalimbali ambayo yanafanywa na benki katika kurudisha Kwa Jamii.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe. Victoria Mwanziva ambaye mgeni rasmi katika Hafla hiyo ameishukuru CRDB benk Kwa kutoa mifuko hiyo ya saruji huku akiwasihii wanafunzi kuhakikisha wanasoma kwa bidii ili waweze kufanya vizuri kwenye masomo yao.
Akipokea mifuko hiyo ya saruji kutoka kwa meneja wa CRDB kanda ya Kusini Mstahiki Meya wa Manispaa ya Lindi Mhe. Frank Magali ameishukuru CRDB Kwa msaada huo ambao unakwenda kusaidia Ujenzi wa uzio Shule.
Sambamba na hilo Magali ameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt, Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kwa kazi kubwa na nzuri anayoifanya hasa Katika Manispaa ya Lindi Mkoa wa Lindi na taifa Kwa ujumla.
Lakini pia ametumia nafasi hiyo kumshukuru Mbunge wa Jimbo la Mchinga Mhe. Salma Rashidi Kikwete Kwa kazi anayoifanya katika kuhakikisha Jimbo hilo linapata maendeleo hususani ni kata ya Kilangala.
katika hatua nyingine katibu wa mbunge Jimbo la Mchinga Abdallah Mkokoi Kwa niaba ya mbunge wa Jimbo hilo ametoa kiasi Cha fedha shilingi laki tano Kwa Wanafunzi wa shule hiyo kwaajili ya kununua futari kwenye mwezi huu wa mfungo.
Ikumbukwe kuwa tarehe 09 Agosti 2024 benki hiyo chini ya meneja wake Kwa kanda ya Kusini ilikabidhi viti na meza 40 shuleni hapo ikiwa ni katika kusaidia kukuza na kuendeleza sekta ya Elimu .
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.