Dkt Catherine amesisitiza kwamba Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania imepanga kuwaunganisha vijana na huduma za kuwainua kiuchumi na huduma za kiuwanagenzi kupitia mradi wa Timiza Malengo awamu ya tatu.
Aidha, katika kufikia lengo la serikali la kudhibiti UKIMWI kama tishio la Taifa ifikapo 2030, TACAIDS imepanga kuendesha kampeni ya TUSONGE NA SAMIA KUTOKOMEZA UKIMWI ili kuongeza kasi ya kitaifa, kikanda na kimataifa ya VVU/UKIMWI ifikapo 2030.
Kampeni hii ni sehemu ya kutambua mchango wa Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania katika Kudhibiti UKIMWI nchini ambapo katika kipindi cha uongozi wake kumekuwa na maboresho makubwa katika upatikanaji wa huduma za kinga, tiba na matunzo ya VVU/UKIMWI na kuongezeka kwa rasilimali za ndani za kwa ajiri ya utekelezaji wa afua za UKIMWI kwa kushirikiana na sekta binafsi kuendesha programu mbalimbali.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.