Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Lindi imetoa taarifa ya tathmini ya ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo 34 yenye thamani ya zaidi ya Tsh. Bilioni 15 katika sekta za afya, maji, na ujenzi katika kipindi cha robo mwaka kuanzia Oktoba hadi Disemba,2024.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Lindi Bi. Asha Kwariko amesema TAKUKURU Mkoa wa Lindi imefanya ufatiliaji wa utekelezaji wa miradi 34 ya maendeleo na kubaini dosari katika miradi 7 yenye thamani ya shilingi billion 9.27.
Aidha Bi. Kwariko ameeleza kuwa, kuelekea uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika October 2025, TAKUKURU Mkoa wa Lindi imejipanga vyema kudhibiti mianya ya vitendo vya rushwa na ufatiliaji wa rasilimali za umma na kuwafikisha mahakamani wale wote watakaobainika kujihusisha na vitendo vya Rushwa.
Sambamba na hayo, TAKUKURU Mkoa inaendelea kujivunia programu ya TAKUKURU Rafiki inayoendeshwa katika kata mbalimbali kwa lengo la kubaini na kutafuta utatuzi wa moja kwa moja wa kero za wananchi katika maeneo yao, hivyo kuwaomba wananchi na wadau wa maendeleo kujitokeza katika mikutano na kuendelea kuwaunga mkono katika kuzuia vitendo vya rushwa kwa kutoa taarifa za viashiria vya rushwa katika chaguzi na miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.