Shirika la Maendeleo ya Petroli ya Tanzania (TPDC ) katika kutekeleza majukumu yake ya utafutaji , uendeshaji, uzalishaji, uchakataji, usafirishaji na usambazaji wa mafuta na gesi asilia kwa niaba ya serikali, imetambulisha mradi wa uchukuaji wa taarifa za mitetemo kwa kamati za ulinzi na usalama za Mkoa na Wilaya ya Lindi leo Julai 15, 2025 katika ukumbi mdogo wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi.
Awali akitambulisha mradi huo Dkt. Shaibu Nuru ambaye ni Meneja mradi wa utafutaji wa mafuta na gesi kitalu cha Lindi na Mtwara, amesema TPDC inafahamu umuhimu wa ushirikishaji katika utekelezaji wa miradi mikubwa kama hiyo .
" tunafahamu umuhimu wa ushirikishaji wa wadau muhimu katika utekelezaji wa miradi mikubwa kama hii kabla ya kwenda kwa jamii kuwafahamisha umuhimu wa mradi na namna ya utekelezaji wake"
Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe. Victoria Mwanziva akizungumza kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi, amesema serikali ipo tayari kwa utekelezaji wa mradi huo mkubwa ambao unakwenda kufanyika katika vijiji Nane vya Halmashauri ya Mtama .
Aidha, Mhe. Mwanziva ametumia fursa hiyo kumpongeza na kumshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuiwezesha TPDC kufanya utafiti wa gesi asili yenyewe pasipo kutegemea wataalamu kutoka nje ya nchi.
Maana ya uchukuaji wa takwimu za Mitetemo (3D Seismitic Data Acquisition ) katika muktadha wa sekta ya mafuta na gesi asili , ni teknolojia ya kisasa inayotumika kutambua uwepo na ukubwa wa akiba za mafuta na gesi chini ya ardhi. Haiwezekani kuanza zoezi la uchimbaji wa gesi au mafuta bila kufanya utafiti wa kutosha.
Zoezi hilo linafanyika kwa kutumia magari maalum yanayotoa mitetemo midogo na vipokezi maalumu vinavyopokea mitetemo hiyo baada ya kurudi kutoka chini ya ardhi, wataalamu wanapata picha ya kina ya miundo ya jiolojia chini ya ardhi.
@wizara_ya_nishati_tanzania
@ortamisemi
@msemajimkuuwaserikali
@gersonmsigwa
@tpdctz
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.