Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mheshimiwa Zainab Telack, ametoa wito kwa vijana na wananchi kwa ujumla kufanya mazoezi mara kwa mara ili kuimarisha afya zao.
Akizungumza katika maonyesho ya madini yanayoendelea katika viwanja vya madini wilayani Ruangwa, Mheshimiwa Telack alieleza kuwa afya ni mtaji mkubwa wa maendeleo na ustawi wa maisha ya kila mwananchi.
"Afya bora ndiyo msingi wa maisha na maendeleo ya mtu binafsi na taifa kwa ujumla. Tunapaswa kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi kila wakati ili kuimarisha kinga ya mwili dhidi ya magonjwa mbalimbali," alisema RC Telack.
Aidha, alihamasisha wananchi kuendelea kujitokeza kwa wingi kushiriki na kujifunza kupitia maonyesho ya madini, ambayo yameleta fursa mbalimbali za kiuchumi na kielimu kwa wakazi wa mkoa wa Lindi na maeneo jirani.
Maonyesho hayo yanalenga kuhamasisha maendeleo ya sekta ya madini na kutoa nafasi kwa vijana kujifunza teknolojia, usindikaji, na fursa za uwekezaji zilizopo katika rasilimali za madini.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.