Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais (Kazi maalum), Mhe. Capt. George Huruma Mkuchika ametoa wito kwa wananchi kujenga utamaduni wa kula vyakula vya asili na kutumia mbegu bora ili kypata matokeo mazuri.
Wito huo ameutoa mapema leo Agost 6, 2025 alipoungana na washiriki wa maonesho ya Nanenane kanda ya kusini katika hamasa ya matumizi ya mbegu za asili na ulaji wa vyakula vya asili.
Waziri Mkuchika ameitaka jamii kuhakikisha wanakula vyakula visivyo hatarishi kwa afya na badala yake kupenda kula vyakula vya asili vyenye lishe bora ili kuweza kustawisha jamii.
Hili kupata matokeo makubwa zaidi Mhe. Kapten Mkuchika amewataka TARI kuona namna ya kupata mbegu bora ambayo inaweza kustahimili magonjwa na kuzalisha korosho bora humu akiwataka wakulima kuzingatia kanuni za kilimo kutoka kwa wataalam ikiwemo aina za dawa na usafi wa shamba.
“Mikorosho ya siku hizi usipopuliza dawa unakosa korosho, tunamshukuru Rais Samia kwa kutupa pembejeo bure, tumeweza kuongeza uzalishaji wa korosho. Niwasihi wakulima wenzangu tupalilie mashamba kwa wakati, tusipalilie kwa moto.”Alieleza Mhe. Mkuchika .
Kwa upande wake Dkt. John Tenga , kaimu Mkurugenzi wa TARI Naliendele ameeleza namna ambavyo wamekuwa wakifanya jitihada kubwa katika kuboresha na kupata mbegu bora zenye matokeo chanya kwa mkulima.
“Tumekuwa tukiwashirikisha wakulima katika tafiti zetu, majibu anayotoa mkulima sisi tunaboresha na kutengeneza mbegu bora zinazompa mkulima tija.” Alieleza Dkt. John Tenga, Kaimu Mkurugenzi wa TARI-Naliendele .
Katika hatua nyingine Mhe. Kapten Mkuchikia amevitaka vyama vya Ushirika kuhakikisha mazao yanayozalishwa kanda ya kusini yanaingizwa katika mfumo wa stakabadhi ghalani (TMX) ili kumhakikishia soko mkulima
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.