Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Mhe. Abdallah Mwaipaya ametoa rai kwa viongozi na wananchi wanaoshiriki na kutembelea maonesho ya nanenae kuwa mabalozi wazuri kwa wengine.
Mhe. Mwaipaya ametoa rai hiyo leo siku ya tatu ya maonesho ya nanenane kanda ya kusini yanayofanyika katika viwanja vya Ngongo, mkoa wa Mtwara.
“Taasisi mbalimbali zipo hapa kwenye maonesho, sisi tuliofika tayari inatakiwa tuwaeleze na wengine ili waweze kuja kujifunza na kuhudumiwa.” Alieleza Mhe. Mwaipaya
Katika ziara yake hiyo, Mhe. Mwaipaya alipata fursa ya kutembelea taasisi mbalimbali za serikali ikiwemo Bodi ya Korosho CBT, VETA, EWURA na kujifunza kuhusu huduma wanazotoa na namna zinavyoweza kuwanufaisha wananchi.
“Chagua viongozi bora kwa maendele endelevu ya kilimo, mifugo na uvuvi”
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.