"TWENDENI TUJITOKEZE KUPIGA KURA
OKTOBA 29, 2025 "
Chief wa Wamwera Mkoa wa Lindi.
Chifu wa Kabila la Wamwera, Ismail Malibiche, amewahimiza wananchi wa Nachingwea kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba
29, 2025, amesisitiza kuwa kushiriki uchaguzi ni haki ya kikatiba na njia muhimu ya kuchagua viongozi bora watakaosimamia maendeleo ya wilaya hiyo.
Aidha, Chifu Malibiche amewakaribisha wananchi kuhudhuria sherehe za kimila zitakazofanyika hivi karibuni, ambazo zitatoa fursa ya kupata elimu kuhusu umuhimu wa uchaguzi kwani elimu hiyo itasaidia kuongeza uelewa na kuimarisha umoja kwa wananchi kuelekea Uchaguzi mkuu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.