UBUNIFU NA UHAMASISHAJI WA WAWEKEZAJI VYAHITAJIKA KUBORESHA SEKTA YA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI LINDI
Lindi, Novemba 25, 2025 – Katika ufunguzi wa kikao kazi cha Maafisa Biashara wa Mkoa wa Lindi, Ndugu Boniface Kidulani, Kaimu Katibu Tawala Msaidizi wa Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, ameipokea kwa uzito wito uliotolewa na Kaimu Katibu Tawala Mkoa Bwn. Mwinjuma Mkungu wakati wa kufungua kikao hicho.
Amesisitiza kuwa maafisa biashara kutoka halmashauri zote za mkoa wanapaswa kuzingatia umuhimu wa ubunifu, uhamasishaji madhubuti wa wawekezaji, pamoja na kuimarisha ushirikiano kati ya wawekezaji, wafanyabiashara, maafisa biashara na wadau wengine muhimu.
Aidha, Ndugu Kidulani ameeleza kuwa ushirikiano huo ni nguzo muhimu itakayowezesha ukuaji na uimara wa sekta ya uchumi mkoani Lindi, ikiwemo kuvutia uwekezaji mpya na kuendeleza biashara zilizopo.






Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.