UJENZI WA BANDARI KILWA WAFIKIA 87.3%
Leo Novemba 28, 2025, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, amefanya ziara ya ukaguzi wa maenndeleo ya mradi wa bandari ya kilwa, unaotekelezwa wilayani kilwa mkoa wa Lindi, katika ukaguzi huo Mhe. Balozi Dkt. Bashiru ameridhishwa na hatua mbalimbali za ujenzi wa Bandari hiyo, ambapo utekelezaji wake umefikia zaidi ya asilimia 87.3%. Hadi sasa, zaidi ya shilingi bilioni 199.3 ambazo ni fedha za ndani, tayari zimelipwa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo.
Akizungumza baada ya ukaguzi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru amepongeza jitihada kubwa ambazo zimefikiwa katika utekelezaji wa mradi huo muhimu.
Katika hatua nyingine, Waziri huyo amewataka viongozi na wawakilishi wa wananchi, wakiwemo Baraza la Madiwani, kuweka mikakati madhubuti itakayowezesha wananchi kunufaika na uwekezaji mkubwa uliowekwa na Serikali.
Aidha, Baada ya bandari hiyo kukamilika Mhe. Balozi Dkt. Bashiru amezitaka mamlaka zitakazohusika na usimamizi wa bandari hiyo kutoa elimu elekezi kwa wananchi ili waweze kunufaika ipasavyo na fursa zitakazotokana na mradi huu.
Aidha, amepongeza wananchi wa Kilwa kwa kuupokea mradi huo kwa moyo mzuri na kuonyesha ushirikiano tangu kuanza kwa ujenzi wa bandari hiyo.
Akisisitiza ushiriki wa viongozi hao, alisema:
"Hatua hii iloyofikiwa kwa vyovyote vile kuna mchango wa baraza la madiwani, baraza la madiwani sasa likae mkao kupanga namna wananchi wa kilwa na wenyeji wa kilwa hasa vijana na akina mama watakavyonufaika na mradi huu." - Mhe. Balozi Dkt. Bashiru.





Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.