Mkuu wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye ni Rais Mstaafu wa Serikali ya awamu ya Nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanznia leo Juni 30, 2025, ametembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam Tawi la Ngongo na Ruangwa Lindi ndaki ya kilimo inayojengwa Ngongo Manispaa ya Lindi na kuridhishwa na hatua iliyofikiwa.
Awali akiwasilisha taarifa Mhandisi Valeria G. Kinyero ambaye ni Msimamizi wa ujenzi wa Chuo hicho upande wa UDSM amesema Mradi wa ujenzi wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam Tawi la Ngongo na Ruangwa – Lindi, unatekelezwa Ngongo Manispaa ya Lindi na Likunja ya Ruangwa. Mradi huo ambao awamu ya kwanza unajumuisha ujenzi wa majengo sita ya Chuo kwa Ngongo na Majengo Matatu ya Chuo kwa Likunja na ujenzi huo unajumuisha miundombinu saidizi ikiwepo Barabara, Maji na Umeme.
Mandishi ameongeza kuwa ujenzi huo unajengwa chini ya usimamaizi wa Geomestry Consultants Limited (Mhandisi Mshauri ) na mradi ulianza kutekelezwa 21/03/2025 na unatarajiwa kukamilika 19/9/2025 .
Mhe. Dkt. Kikwete amepongeza na kuridhishwa na hatua hiyo ya ujenzi na kusisitiza kuendelea kuongeza kasi ya ujenzi kwa kuzingatia viwango na kuwataka uongozi wa Manispaa ya Lindi kuanza utaratibu wa kupima viwanja vyote vinavyozunguka eneo hilo la Chuo.
Ujenzi wa Chuo hicho hadi kukamilika kwake unatarajiwa kugharimu bilioni 13, hadi kufikia sasa mkandarasi ameshalipwa bilioni 4.7.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.