Ujenzi wa jengo la kibiashara "Mtanda Commercial Complex " linalojengwa Manispaa ya Lindi kwa thamani ya Tsh Bilioni 4.2 chini ya Shirika la Nyumba la Taifa (National Housing Corporation ) NHC umefikia 40% tangu ulipoanza Julai 1, 2024 hadi leo Februari 13, 2025.
Akieleza hatua za ujenzi wa jengo hilo Mhandisi Martha Noel Kabia amesema kuwa ujenzi wa jengo hilo kubwa la kibiashara hadi sasa umefikia 40% tangu ulipoanza Julai 1, 2024 na unatarajiwa kukamilika Desemba 31, 2025.
Ikumbukwe kuwa ujenzi wa jengo hilo kubwa la kibiashara ni mpango wa serikali katika kudumisha ustawi wa wananchi katika shughuli mbalimbali ikiwemo kukuza uwekezaji wa ndani.
Baadhi ya huduma ama shughuli ambazo zinatarijiwa kupatikana katika jengo la Mtanda Commercial Complex pamoja na huduma za kibenki, huduma za chakula, Maduka zaidi ya 40 ya bidhaa mbalimbali , Baa na Supermakert .
Ujenzi wa mradi huu kwasasa unatoa fursa kwa wananchi wenye ujuzi mbalimbali kupata ajira za muda zikiwemo kuuza chakula na kazi za kusaidia mafundi. Mradi huu utakapokamilika unatarajiwa kutoa fursa nyingi za kiuchumi ikiwemo ajira.
Mmoja wa wafanyakazi katika ujenzi wa mradi huo Ndugu John Haktibu ameshukuru kuwa miongoni mwa waliopata fursa ya ajira za muda na kuahidi kufanya kazi kwa juhudi ili kufanikisha lengo la serikali.
Naye, Bi. Asha Said Mbinga, mfanyakazi katika mradi huo ameipongeza serikali kwa mradi, kwani licha ya kutoa ajira kwa wananchi, unatoa fursa za kibiashara na kuleta mandhari ya mji wa Lindi.
Kwa upande wake fundi Mkuu wa mradi huo Mhandisi Hassan Magawa amepongeza namna shirikia la Nyumba NHC lilivyojipanga katika utekelezaji na usimamaizi wa mradi huo kwani tangu ujenzi ulipoanza hakuna changamoto yoyote iliyojitokeza katika hatua mbalimbali za ujenzi na ndiyo maana linakwenda kwa kasi na ubora .
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.