Shirika la Maendeleo la Petroli Tanzania (TPDC) kwa kushirikiana na Equinor na Shell ambao ni wawekezaji wa mradi wa uzalishaji na usindikaji wa Gesi Asilia Tanzania (TLNG) wameendeleza ujenzi wa shule ya msingi Likongo unaogharimu kiasi cha Bilioni 1.2.
Akizungumza mara baada ya kutembelea majengo ya shule hiyo Mhandisi Burhan Omary amesema kuwa mradi huo wa shule ya msingi Likongo utagharimu zaidi ya Bilioni 1.2 ambao unatarajiwa kukamilika Desemba 27, 2025 ambapo hafi sasa umefikia 53%.
Mhandisi Omary ameendelea kusema kuwa ujenzi wa shule hiyo utakuwa na madarasa 9,na madarasa mawili ya shule ya awali nyumba za walimu pamoja na jengo la utawala.
"Mradi huu utakapo malizika utagharimu zaidi ya Sh.1.2 Bilioni na hadi sasa tumeweza kuajiri wafanyakazi wazawa wapatao 107, pia ujenzi wa shule hii ukikamilika
utakuwa umemaliza changamoto ya elimu katıka eneo hili kwani walimu watakuwa wanaishi hapa hapa shuleni, kuliko ilivyosasa walimu wanatoka mbali kuja kufundisha hapa Likongo."amesema Mhandisi Omary.
Naye Ofisa maendeleo mwandamizi kutoka TPDC Ally Mluge amesema kuwa lengo la TPDC ni kutoa ushirikiano kwa serikali na kurudisha kwa jamii kama kuboresha miundombinu mbalimbali ikiwemo shule .
"Tumekuwa na kawaida ya kurudisha kwa jamii katika kuboresha miundombinu mbalimbali kama shule na kutoa ushirikiano kwa serikali katika kuleta maendeleo. "amesema Mluge.
Mwenyekiti Renatus Nyanda akiongozana na kamati ya CSR amesema kuwa ujenzi wa mradi wa shule ni mradi wa mfano kwani utachochea ukuaji wa elimu katika eneo la Likong’o.
"Niwahakikishie wananchi wa Likong’o kuwa ifikapo 2026 watoto wenu wataanza kusoma katika shule hii mpya, napia niwapongeze sana wasimamizi wa mradi, csr tumelidhishwa na maendeleo ya mradi huu." amesema Nyanda.
Mkuu wa Wilaya ya Lindi Victoria Mwanziva amewashukuru na kuwapongeza TPDC kwa kuweza kuboresha mazingira ya elimu pamoja na kuinua hadhi ya shule.
"Tunawashukuru sana TPDC kwa kuweza kurudisha kwa jamii na kutuboresha mazingira ya shule yetu imani yangu kwenu mradi utakamilika kwa wakati na ifikapo 2026 wanafunzi wa darasa la awali wataanza kuyatumia madarasa yao."amesema Mwanziva.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.