Kikao cha tatu cha maandalizi ya Maonesho ya wakulima maarufu Nanenane yaMwaka 2025 Kanda ya Kusini Ngongo Lindi, kimefanyika katika ukumbi wa JKT Ngongo Mkoani Lindi huku wadau wakisisitizwa kulipa ada ya ushiriki kwa wakati .
Kikao hicho kikiongozwa na Ndugu Mwinjuma Mkungu ambaye ni katibu Tawala msaidizi seksheni ya Uchumi na Uzalishaji Lindi akiambatana na Makamu mwenyekiti ambaye ni Mkuu wa seksheni ya Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Mtwara.
Wamesisitiza suala la utoaji wa michango ya ada ya ushiriki kwa wadau ambao ni taasisi za umma na binafsi, Halmashauri zote za mikoa ya Lindi na Mtwara kabla ya Julai 20, 2025.
Ndugu Mkungu amesema kuwa kufana kwa maonesho hayo kunategemea sana michango hiyo kutolewa kwa wakati.
Kauli mbiu ya Maonesho hayo ya 2025 inasema “Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi 2025 “
#tukutaneNgongolindi
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.