Kwa mujibu wa Kanuni ya 15(20)(c) ya Kanuni za Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura za mwaka 2025, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imeweka utaratibu maalum wa kuwawezesha wanafunzi na wafungwa waliohukumiwa kifungo cha chini ya miezi sita pamoja na mahabusu kuandikishwa kama wapiga kura.
Hatua hii inalenga kuhakikisha kuwa makundi hayo yanapata fursa ya kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kidemokrasia, sambamba na haki yao ya kikatiba ya kushiriki uchaguzi.
Bi. Giveness Aswile, Mkurugenzi wa Habari na Elimu ya Mpigakura ameeleza kuwa vituo 140 nchini tayari vimeshasajiriwa kwa ajiri ya kuhudumia makundi hayo ambapo kwa upande wa Tanzania Bara, jumla ya vituo 130 vya kuandikisha wapiga kura vimeanzishwa ndani ya magereza huku kwa upande wa Zanzibar, vituo 10 vya kuandikishia vimewekwa kwenye vyuo vya mafunzo.
Utaratibu huu unathibitisha dhamira ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ya kuhakikisha kuwa kila Mtanzania mwenye sifa kisheria anapata fursa ya kushiriki katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 ikiwemo wale walioko katika maeneo ya magereza na vyuo vya mafunzo
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.