• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Lindi Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Lindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Sehemu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Menejimenti ya Serikali za Mtaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Kilwa
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Lindi
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Liwale
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Nachingwea
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Ruangwa
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa
    • Halmashauri ya Manispaa ya Lindi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Lindi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Liwale
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma ya Maji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Jarida
    • Fomu
    • Sheria
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Habari

WAKULIMA WA MWANI KILWA MASOKO KUPATIWA MSAADA NA SERIKALI.

Posted on: September 13th, 2021

Leo wanachama wa chama cha ushirika cha wakulima wa mwani wanaofanya shughuli ya ukulima wa mwani mji mdogo wa Kilwa Masoko wamepata faraja baada ya kutembelewa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega alipofanya ziara yake Mkoani Lindi.

Mhe. Naibu Waziri amekutana na wanachama hao alipotembelea kiwanda kidogo cha Kampuni ya Mwani Mariculture kilichopo Kilwa Masoko  kinachochakata na kufungasha zao la mwani kabla ya kusafirisha kwenda sokoni.

Mhe. Naibu Waziri akiwa kwenye kiwanda hicho alizungumza na wakulima wa zao hilo linalolimwa kwa asilimia kubwa na wanawake, Wakulima  walieleza changamoto wanazokabiliana nazo katika kilimo cha mwani ambazo ni pamoja na ugumu wa upatikanaji pembejeo ikiwemo kamba, taitai pamoja na bei ndogo ya Tsh. 500 kwa kilogramu 1 ya mwani.

Akiipongeza kampuni ya Mwani Mariculutre kwa kuendelea kununua mwani wa wakulima wa Kilwa Masoko, Mhe. Abdallah Ulega amewaomba wakulima hao kulima kwa wingi mwani aina ya cottonii ambao unahitajika kwa kiasi kikubwa sokoni na bei yake ni nzuri takribani Tsh. 1,500 kwa kilogramu moja huku akiwaahidi kuwaletea mbegu bora ya aina hiyo ya mwani.

Pamoja na ahadi za uwezeshwaji wa mbegu bora, Mhe. Abdallah Ulega amewaahidi wakulima hao kuwawezesha kamba pamoja na vichanja bora vya kuanikia mwani vyenye ukubwa mpaka mita 100 ili watunze ubora wa zao hilo kwa kutoanika chini.

Katika kuhakikisha ahadi hizo zinatekelezwa aliwaagiza viongozi na wataalam wa Idara ya Ukuzaji Viumbe Maji alioambatana nao kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi kukaa na viongozi wa Chama cha Wakulima wa mwani Kilwa Masoko ili kupitia nyaraka zao na kuanza mara moja utekelezaji wa kukiwezesha chama hicho.

Matangazo

  • WANAFUNZI WALI0CHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2021-MKOA WA LINDI March 29, 2021
  • Vitabu vya kalenda za utekelezaji wa mitaala ya Elimu ya Awali, Msingi na Sekondari February 08, 2022
  • FOMU ZA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO KWA MKOA WA LINDI 2022 May 09, 2022
  • FOMU ZA MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SHULE YA SEKONDARI KWA MKOA WA LINDI (JOINING INSTRUCTIONS) December 16, 2020
  • tazama zote

Habari Mpya

  • JAMII NA WAZAZI WATAKIA KURUDI KUBEBA JUKUMU LA MALEZI KWA WATOTO

    May 03, 2025
  • MKUU WA MKOA WA LINDI AONGOZA KIKAO CHA LISHE NGAZI YA MKOA

    May 03, 2025
  • MHE. TELACK AZINDUA MPANGO MKAKATI WA ELIMU MKOA WA LINDI KWA MWAKA 2025

    May 02, 2025
  • RC TELACK AKABIDHI TUZO ZA ELIMU KWA WALIMU,WANAFUNZI NA HALMASHAURI ZILIZOFANYA VIZURI MKOANI LINDI.

    May 02, 2025
  • tazama zote

Video

CWT WASHAURIWA KUMALIZA MIGOGORO YA CHAMA CHAO MAPEMA ILI KUWAPA UTULIVU WANACHAMA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Watumishi Portal
  • Kilwa District Council
  • Nachingwea Disctrict Council
  • Ruangwa District Council
  • Liwale District Council
  • Lindi Municipal
  • Lindi District Council

Kurasa mashuhuri

  • Public Procurement Reguratory Authority
  • Tamisemi
  • e-Government Agency
  • Watumishi Portal
  • Sekretarieti ya ajira
  • CWT WASHAURIWA KUMALIZA MIGOGORO ILI WANACHAMA WAPATE UTULIVU

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi

    Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi

    Simu: 023-220-2098

    Rununu:

    Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.