WAKULIMA WA MWANI LINDI WAPEWA MAFUNZO NA UMUHIMU WA KUJIUNGA NA USHIRIKA.
Vikundi vinne vya wakulima wa zao la Mwani Halmashauri ya Mtama Mkoani Lindi wamepata mafunzo yanayohusu kilimo hicho na umuhimu wa kujiunga ushirika.
Mafunzo hayo ambayo yameratibiwa na Ofisi ya waziri Mkuu Sera bunge na uratibu yamefanyika Novemba 19, 2025 katika ukumbi wa Ofisi za CWT Mkoa wa Lindi.
Afisa Uvuvi Mkoa wa Lindi Ndugu Jumbe Kawambwa ambaye mgeni rasmi wa kikao kazi hicho amesema , mafunzo hayo yatakwenda kuleta tija kubwa sana kwa wakulima wa mwani Mkoani Lindi kwani faida za kujiunga na ushirika ni nyingi sana
"Kupitia mradi huu tunatarjia kuongeza vyama vinne vya ushirika ambavyo ni Mongomongo, Shuka, Mmumbu na Sudi kutoka halmashauri ya mtama ambao watakwenda kuona manufaa mengi ya kujiunga na ushirika ikiwemo kupata wadau na vifaa mbalimbali" Amesema ndugu Kawamba.
Kawamba ameongeza kuwa uwepo wa wadau na vyama vya ushirika kumesaidia sana kuongezeka kwa uzalishaji wa zao la mwani kutoka kilo Mia tisa hadi tani Elfu Tatu huku matarajio kufika tani elfu sita.
Aidha , ametoa wito kwa wakulima wa mwani kuendelea kujiandaa na kujiweka sawa katika kuiendea hatua hiyo kubw yenye manufaa.
Kwa upande wake Mratibu wa mafunzo hayo ndugu Godfrey Christopher ambaye ni mratibu wa viumbe maji katika mradi wa kuimarisha upatikanaji wa lishe kwa wakulima wadogo wa samaki na Mwani kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, amesema mafunzo hayo yanalengo la kuwajengea uwezo wakulima wadogo wa zao la mwani kutoka vijiji Vinne ambavyo ni Shuka, Mongomongo, Mmumbu na Sudi ambapo kila kijiji kimetoa wawakilishi watano na kufanya jumla ya wawakilishi 20.
"Lengo la mafunzo haya kuwajengea uwezo wakulima wadogo wa mazao ya mwani katika kujiandaa kujiunga na ushirika ili waweze kuona tija wa shughuli wanayoifanya " Ndugu Godfrey Mratibu.
Mafunzo hayo yamefanyika kwa siku saba ambapo wanufaika wameishukuru serikali kwa muongozo ambao wanaendelea kuutoa ili wananchi wake wanufaike na rasilimali zilizopo nchini katika kujiinua kiuchumi.






Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.