WAKULIMA WATAKIWA KUJISAJILI NA KUUZA MAZAO KATIKA USHIRIKA.
Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na uzalishaji Mali Mkoa wa Lindi Ndugu Mwinjuma Mkungu ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Lindi kuona umuhimu wa kujisajili katika mifumo ya kiserikali ambayo inasaidia kupata takwimu sahihi zinazorahisisha kupata pembejeo kwa kiwango kinachohitajika. Wito huo ameutoa Novemba 18, 2025 katika hafla ya kupokea na kukabidhi mbegu bora za ufuta pamoja na kuzindua msimu mpya wa kilimo 2025/2026 katika viwanja vya Ngongo Manispaa ya Lindi.
“Nitoe wito kwa wakulima wote, ni vizuri sasa kila mkulima kujisajili katika mifumo ya kiserikali na kuuza mazao yao katika ushirika ili kupata takwimu sahihi zitakazo rahisisha kupata pembejeo za ruzuku zinazoendana na uhalisia “ Ndugu Mkungu.
Aidha, Mkungu ametumia fursa hiyo kuwahamasisha wananchi kuona umuhimu wa kulichukua zao la choroko kwa umuhimu mkubwa ambalo litaongeza mzunguko wa fedha na kipato kwa mkulima na serikali.
“ zao la Choroko ambalo limeshaanza kwa baadhi ya maeneo linapswa sasa kuongeza nguvu kulimwa katika maeneo yetu yote, kwa kufanya hivyo tutakuwa na mazao manne ya biashara katika mkoa wetu na hivyo kuongeza mzunguko wa fedha kwa mmoja mmoja na serikali “ Aliongeza Ndugu Mkungu .
Ikumbukwe kuwa Mkoa wa Lindi unamazao makuu matatu ya kilimo ambayo ni korosho, Ufuta na Mbaazi ambayo yamekuwa yakiingizia fedha nyingi Mkoa wa Lindi.






Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.