Maelfu ya wananchi wamepokea kwa shauku fursa ya kupata elimu ya haki za kisheria pamoja na msaada wa sheria bure kupitia Kampeni ya Msaada wa sheria ya Mama Samia (Mama Samia Legal Aid Campgain) iliyozinduliwa leo Mkoani Lindi na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kupitia Kampeni hiyo, inayotarajiwa kudumu kwa muda wa siku tisa katika ngazi za Kata na Vijiji huku ikilenga zaidi katika kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu masuala ya kisheria na kusaidia kutatua changamoto na migogoro inayohusiana na ardhi, ndoa, mirathi na haki za binadamu na utawala.
Mhe. Majaliwa amewasisitiza watumishi wa serikali wanaokwenda kuwahudumia wananchi kupitia kampeni hii, kutoa huduma za msaada wa kisheria kwa ufanisi bila ubaguzi ili kuweza kufikia kutimiza adhima ya serikali na kampeni hii ya kuongeza wigo wa uelewa wa sheria kwa wananchi.
Aidha, Mhe. Majaliwa ameeleza kuwa serikali imeendelea kuboresha miundombinu ya nyumba za utoaji wa haki ikiwemo mahakama za mwanzo na wilaya, ofisi za mashtaka za wilaya ili kurahisisha zoezi la utoaji haki na kuepuka mlundikano wa kesi.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Jumanne Sagini, amesema utekelezaji wa kampeni hii ni mahsusi kwa kuleta unafuu na kuongeza uelewa wa kisheria na haki za binadamu kwa umma, elimu ya sheria na wananchi kuamini utatuzi wa migogoro kupitia njia ya mbadala kwa kuzingatia misingi ya utawala bora.
Mwakilishi wa Rais waChama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Bwana. Ipilinga Panya amesema kuwa kwa kuzingatia Kifungu cha 4 kinachoelezea kulinda na kutetea wananchi katika mambo yanayohusu sheria, TLS inaungana na Wizara ya Katiba na Sheria kutoa elimu za huduma za kisheria ili kusaidia upatikanaji wa haki na misaada ya kisheria.
Vilevile, wananchi wamehamasishwa kujitokeza kwa wingi ili waweze kunufaika na uwepo wa kampeni hii, kuhakikisha migogoro yao inashughulikiwa kisheria ili kuweza kuishi kwa amani na kuweza kuendelea na shughuli za kimaendeleo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.