Wizara ya Katiba na Sheria kwa kushirikiana na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) wametakiwa kuongeza kasi ya utoaji elimu kwa jamii kuhusu umuhimu uandikaji wa wosia na njia ya ugawaji wa mirathi ili kupunguza migogoro ya kifamilia inayoibuka wakati wa zoezi la ugawaji wa mali.
Agizo hilo limetolewa na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati akizindua Kampeni ya Msaada wa Sheria ya Mama Samia Mkoani Lindi leo Februari 19, 2025 katika viwanja vya madini, wilayani Ruangwa.
Aidha, Mhe. Majaliwa amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika kambi za kampeni hii zitakazokuwa zinaendeshwa katika kila Halmashauri kwa muda wa siku 9 ili kuweza kupata elimu inayohusu mirathi, uandaaji na uhifadhi wa wosia pamoja na huduma nyingine za misaada ya kisheria itakayokuwa inatolewa bila malipo yoyote.
Pia, Waziri Mkuu amewataka wananchi kuachana na dhana potofu ya kuamini kuwa kuandaa usia ni uchuro wa kujitabiria kifo kwani ni njia salama ya kuondoa migogoro inayoweza kuibuka ambapo kwa asilimia kubwa waathirika wake huwa ni akinamama na watoto.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.