Wizara ya Maji kupitia Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Lindi kwa kushirikiana na Kanisa la Anglikana Tanzania Dayosisi ya Masasi chini ya ufadhili wa shirika la Grille Foundation wanatekeleza mradi wa maji wa Chikombe-Mkanga Il ambao ni wa upanuzi wa miundombinu kutoka mradi mkubwa wa Rondo kwaajili ya kuwahudumia wananchi wote
Mradi huo unatarajiwa kuhudumia Jumla ya wakazi 2823 kutoka vijiji vya Chikombe na Mkanga Il vilivyopo Tarafa ya Rondo, Kata ya Mnara- Halmashauri ya Mtama, wanatarajia kupata neema kubwa ya upatikanaji wa maji safi, salama na yenye kutosheleza muda wote.
Wananchi wa Rondo- wameshiriki katika hatua zote za utekelezaji wa mradi huu haswa kwenye mazoezi ya ufukiaji wa mabomba, na wameahidi utunzaji wa miundombinu ya maji ya mradi ambao unatazamiwa kukamilika hivi karibuni.
Wananchi hao, wanazidi kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa jitihada kubwa za kuendelea kutatua changamaoto zao zikiwemo katika sekta ya Afya , Elimu ,barabara na Huduma ya Maji.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.