Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack na Kamishna wa Tume ya Maendeleo ya ushirika ametoa rai kwa Wanaushirika kuendeleza Ushirikiano miongoni mwao na kuchapa kazi ili kujiletea maendeleo.
Amesema hayo wakati wa Hafla ya Futari iliyoandaliwa na Tume kwa Watumishi wake Machi 25, 2025 Jijini Dodoma.
Mhe. Telack amebainisha kuwa tunapoelekea misimu ya mazao ni muhimu kila mtumishi atimize wajibu wake kwa weledi na bidii ili kujenga Ushirika na kuwahudumia Wakulima ipasavyo.
Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume Dkt. Benson Ndiege amewashukuru Menejimenti na Watumishi na kuahidi kuendelea kusimamia Ushirikiano, uweledi na ufanisi katika utendaji wa Tume.
Hafla hiyo imehudhuriwa na Makamishna wa Tume, Watumishi wa Benki ya Ushirika, Wajasiriamali na wadau mbalimbali.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.