WATAALMU WA KILIMO NA UFUGAJI LINDI WATAKIWA KUONGEZA UZALISHAJI WA MAZAO YA BIASHARA.
Wataalamu wa sekta za kilimo na ufugaji Mkoa wa Lindi wametakiwa kuongeza jitihada za kusimamia uzalishaji wa mazao ya biashara kama ufuta, choroko na korosho pamoja na uzalishaji wa mazao ya chakula ili kuhakikisha upatikanaji wa vyakula na kuinua vipato vya wananchi. Hayo yameelezwa na Katibu Tawala Msaidizi, Uchumi na Uzalishaji Ndugu. Mwinjuma Mkungu alipokua anafungua kikao kazi cha kujadili Mpango wa Maendeleo ya Kilimo Mkoa wa Lindi, kilichowakutanisha maafisa kilimo na ufugaji wa Halmashauri zote za Mkoa wa Lindi. “Tuna mabonde mengi mazuri kwa kilimo cha mazao ya bustani na mboga mboga ambayo wananchi wetu tunaowahudumia tukiwahamisha vizuri na wakajikita katika mazao hayo pia watajipatia tija ya uhakika wa chakula kwa ajiri ya familia zao hivyo fedha watakayopata kupitia mazao ya biashara ikiwemo korosho, ufuta na mbaazi zitatumika kuboreshea hali zao za maisha badala ya kutumia yote kununulia chakula” Aidha, ndugu. Mkungu amehimiza uanzishwaji wa mashamba darasa yatakayotumika kama mfano kwa wananchi kujifunza namna ya uzalishaji wa mazao ambayo hayakuwahi kulimwa kabla ikiwemo Alizeti sambamba na ushirikiano na taasisi nyingine za kilimo zinazojihusisha na utafiti wa mbegu bora za mazao ikiwemo TARI ili kuhakikisha wakulima wanapata mbegu bora zitakazoleta tija katika uzalishaji. Kikao kazi cha kujadili maendeleo ya kilimo katika Mkoa wa Lindi kimelenga kuangazia mwenendo wa uzalishaji wa mazao ya biashara pamoja na chakula kama sehemu ya kuboresha hali ya kimaisha ya wananchi kiuchumi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.