Kwa kutambua umuhimu wa CHW's,Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Grace Magembe amesema kuwa serikali itaendelea kutekeleza mpango kwa kutoa mafunzo kwa watoa huduma za afya ngazi ya jamii zaidi ya laki moja na elfu 37 kwa kipindi cha miaka mitano pamoja na kuweka mazingira wezeshi ili waendelee kufanya kazi zao kwa ufanisi.
Akizungumzia mchakato wa kuwapata Wahudumu wa afya ngazi ya jamii, Dkt. Grace Magembe amesema Wahudumu hao huchaguliwa na wananchi katika maeneo yao wanayoishi katika vitongoji au mitaa kisha Wizara kuwapatia mafunzo ya darasani kwa muda wa miezi sita kwa nadharia na vitendo.
"Wahudumu hawa leo wapo tayari kwenda kutoa huduma kwa wananchi, na hapa watakabidhiwa vitendea kazi vitakavyotumia ikiwemo vishikwambi (tablets), vifaa tiba ikiwemo vifaa vya kupima joto, sukari, presha, uzito na vipeperushi vya elimu za afya. Hii yote ni sehemu ya kuwarahisishia utendaji wenu wa kazi na kuhakikisha mnaimarisha huduma za afya na kinga ndani ya jamii"
Aidha, amewasisitiza watoa huduma hao kutoa huduma kwa wananchi bila upendeleo, na kwa kuzingatia usiri wa taarifa za wagonjwa watakaowahudumia.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.